Secretary General, DOWUTA P.O.Box 7262 Pemba street near National Stadium Temeke Dar es Salaam Tanzania info@dowuta.or.tz
12-05-2025
Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari Tanzania (DOWUTA) kinaundwa na wafanyakazi wa Sekta ya Meli na Bandari Nchini Tanzania. Kuundwa kwa Chama hiki kunashabihiana na mabadiliko ya Kisiasa Kiuchumi na Kijamii. Mabadiliko ya Sera za Uwekezaji, Utandawazi, Uhuru wa kuunda na kujiunga na vyama vya wafanyakazi na mabadiliko ya mazingira ya kazi, kwa pamoja yamesababisha wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi kubuni na kutumia mbinu mpya katika harakati za kudai, kulinda na kutetea haki na maslahi yao nchini Tanzania. Kwa kuwa wafanyakazi Wanatambua kwamba mapambano ya kudai, kulinda na kutetea haki na maslahi yao yanahitaji chombo madhubuti cha uongozi kinachounganisha fikra na vitendo vyao, kwa pamoja wameamua kuunda chombo madhubuti (DOWUTA) kwa madhumuni ya kusimamia maslahi ya wafanyakazi wa shughuli za Meli na Bandari Tanzania.
SHERE ZA MEI MOSI KIGOMA
SHEREHE ZA MEI MOSI KIGOMA.
MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI - KIMKOA KIGOMA WILAYA YA…